Michezo

Yanga SC yamsimamisha kazi Katibu Mkuu

on

Kamati ya utendaji ya Yanga SC imemsimamisha kazi kaimu katibu mkuu wao na Mkurugenzi wa sheria na wanachama wakili Patrick Simon ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Bado haijawekwa wazi moja kwa moja ni tuhuma zipi hasa zinamkabili wakili Patrick lakini Inaaminika kuwa ni miongoni mwa zile zinazotolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mwinyi Zahera.

Hivi karibuni video ya Zahera ilisambaa na kumtuhumu kuwa wakili Patrick amekuwa akitoa majibu sio mazuri kwa FIFA kitu ambacho kinaweza kuigharimu Yanga, inasemekana Zahera bado anaidai Yanga na kesi iko FIFA.

Soma na hizi

Tupia Comments