Michezo

Yanga SC yamtangaza msaidizi wa Eymael

on

Ikiwa ni siku chache zimepita toka uongozi wa Yanga SC kupitia kwa mdhamini wake GSM Tanzania kumtangaza Luc Eymael raia wa Ubelgiji kama kocha wao mpya.

Leo Yanga SC imemtangaza aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ya wanawake Riedoh Berdien kuwa kocha wao wa viungo na kocha msaidizi namba 2.

Riedoh aliwahi kufanya kazi na Luc Eymael katika club ya Free State Stars ya Afrika Kusini, hivyo inatajwa kuwa kaajiliwa Yanga SC kwa mapendekezo ya kocha mkuu Eymael ambaye amewahi kufanya nae kazi.

Soma na hizi

Tupia Comments