Michezo

Yanga SC yamtolea ufafanuzi Kabwili tuhuma zake Simba SC

on

Club ya Yanga SC kupitia kwa afisa habari wake Hassan Bumbuli leo ameongea na waandishi wa habari za michezo na kulitolea ufafanuzi suala la golikipa wao Ramadhan Kabwili, kuwa aliwahi kushawishiwa na Simba SC apewe IST ili ajipatishe kadi ya tatu ya njano.

“Mchezaji wetu (Kabwili) ambaye amekuwa headlines kwa kuzungumza na kituo kimoja cha radio hapa Dar es Salaam, sisi kama club tumemuita Kabwili tukae nae atueleze kinaga ubaga kwa sababu yeye alipokuwa anazungumza Kabwili alikuwa anazungumza historia”

“Sidhani kama mtu anaweza kukuhukumu kwa kuzungumzia historia kwa sababu malalamiko rasmi ya suala alilolisema Kabwili yalitolewa tarehe 12/02/2019 na kocha Mwinyi Zahera, kwa hiyo hatua zingechukuliwa pale, mchezaji wetu ambao alikuwa anatoa historia yake na uzoefu wake kucheza mechi kubwa”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ramadhani Kabwili hivi karibuni katika mahojiano yake na moja kati ya kituo cha radio hapa nchini, alidai kuwa aliahidiwa na kiongozi wa Simba ajitafutie kadi ya 3 ya njao kwa makusudi ili akose mchezo unaofuata vs Simba, kwa kufanya hivyo angepewa zawadi ya gari (Toyota IST).

Soma na hizi

Tupia Comments