Michezo

Yanga SC yaondoka na point moja vs Mbeya City

on

Club ya Yanga SC iliyosafiri kutoka Dar es Salaam hadi jijini Mbeya kucheza mchezo wake wa 9 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji Mbeya City wamekumbana na ugumu kupata matokeo.

Yanga wakiwa Mbeya wameondoka na point moja baada ya mchezo huo kumalizika 0-0 kutokana na timu hizo kukamiana na kucheza kwa tahadhari kubwa ili kuepuka kuruhusu goli.

Sare ya Yanga na Mbeya City inaifanya Yanga kufikisha jumla ya michezo 9 wakiwa nafasi ya 9 kwa kuwa na point 17, wakati Mbeya City wakiwa nafasi ya 18 wakiwa wamecheza game 13 na kufikisha jumla ya point 9.

Soma na hizi

Tupia Comments