Michezo

Yanga SC yaondoka na point Samora

on

Baada ya bodi ya Ligi kushindwa kuruhusu game ya Yanga na Tanzania Prisons ichezwe katika uwanja wa Sokoine Mbeya kwa sababu kuharibika kwa Tamasha la muziki kufanywa katika uwanja huo.

Game hiyo ililazimika kuhamishiwa katika uwanja wa Samora Iringa na kupigwa leo December 27 2019, game hiyo ambayo Yanga walikuwa wanailalamikia kwa kuwagharimu pesa nyingi kutokana na kuhamishwa ghafla.

Yanga wamefanikiwa kuondoka na point tatu kufuatia ushindi wa goli 1-0 lilofungwa na Sibomana dakika ya 5 ya mchezo, Yanga point hizo zinawaweka nafasi ya tatu kwa kuwa na point 21 wakicheza game 10.

Soma na hizi

Tupia Comments