Michezo

Yanga SC yapata kocha mpya raia wa Ubelgiji

on

Uongozi wa Yanga SC leo umemtangaza Luc Eymael kuwa kocha wao mpya mkuu, hiyo ni baada ya kumfuta kazi Mwinyi Zahera.

Luc Eymael ,60, atawasilia Tanzania leo na kwenda Zanzibar kuungana na timu kwa ajili ya kuona maendeleo yake katika michuano ya Mapinduzi Cup nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga bado hawajaweka wazi wamempa mkataba wa muda gani, Eymael ambaye ana uzoefu wa soka la Afrika kwa kufundisha vilabu vya Rayon Sports, AFC Leopard, AS Vita, Polokwane na Free State analetwa kwa ufadhili wa mdhamini wa Yanga kampuni ya GSM.

Soma na hizi

Tupia Comments