Michezo

Yanga yaingia makubaliano na benki TPB kuja na huduma hii….

on

tpbKlabu ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.

Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta  nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.

“Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama” alisema Deo.

Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.

Naye Makaumu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu zitaweza  kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.

Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.

Tupia Comments