Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Borniface Mkwasa ameamua kufanya maamuzi ya ziada baada ya klabu za Azam FC na Yanga kutowaruhusu wachezaji wake kujiunga na kambi ya Taifa Stars August 9 na badala yake kuendelea na maandalizi yao ya mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa August 22.
Mkwasa amelazimika kuita wachezaji wapya kumi ili kuendelea na program yake ya mazoezi kama kawaida hivyo hao ambao hawajaruhusiwa kujiunga atawaangalia katika mechi ya Ngao ya Hisani kwani hawezi kumchukua mchezaji ambae hayuko vizuri na labda ana majeruhi ndio maana aliitisha kambi ya siku kadhaa kablaa ya wachezaji kurejea katika vilabu vyao
“Nafikiri ndio hivyo kwa sababu tulitarajia kwamba wiki hii pengine itakuwa sio wiki muhimu sana kwao kwa sababu wana wiki moja mbele ya maandalizi kwa wiki ijayo lakini hatuwezi kuwalazimisha kwa sababu Tanzania ina wachezaji wengi na sisi tuna bank ya wachezaji kama wamewazuia basi tutawachukua wengine kama unavyoona”>>>Mkwasa
Mkwasa alitangaza kikosi cha timu ya taifa Ijumaa ya August 7 hivyo wachezaji wote wanaocheza Ligi ya ndani walitakiwa kuripoti siku ya Jumapili ya August 9.
Wachezaji walioongezwa kikosini ni golikipa Saidi Mohamed, Vicent Andrew, kutoka Mtibwa Sugar, Mohamed Hussein (Tshabalala) na Ibrahim Ajib, kutoka Simba, Hamis Ally na Juma Mbwana kutoka KMKM, Tumba Swed kutoka Coast Union, Samwel Kamuntu kutoka JKT Ruvu na Ibrahim Hilka kutoka klabu ya Zima moto ya Visiwani Zanzibar sambamba na golikipa wa Tanzania Prisons Mohamed Yusuph ambae bado hajawasili kikosini.
Zaidi Mkwasa ameongea hapa
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos