Michezo

Taarifa ya kuzuiliwa kwa mashabiki kwenye mchezo wa Yanga vs Al Ahly Cairo

on

MBIOOOOMchezo wa marudiano wa michuano ya CAF Champions League baina ya klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Al Ahly ya Misri utachezwa kwenye uwanja usiokuwa na mashabiki, imethibitishwa na mamlaka za usalama na chama cha soka cha nchi hiyo.

Yanga na Al Ahly ambao walichuana wikiendi iliyopita katika mchezo wa kwanza katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam, kwenye mchezo ambao uliisha kwa Yanga kushinda 1-0. Timu hizo zitarudiana jumapili wiki hii.

Hata hivyo habari nzuri kwa Yanga na mbaya kwa Al Ahly, ni kwamba mchezo huo hautokuwa na mashabiki kutoka na sababu za kiusalama.

Azmi Megahed, msemaji wa chama cha soka nchini  Misri, amesema mashabiki hawatoruhusiwa kuhudhuria mechi hiyo kutoka sababu za kiusalama.

Jumamosi wiki iliyopita, polisi walipambana na mashabiki wa Zamalek White Knights ambao walijaribu kuingia katika uwanja wa Cairo kuangalia mchezo kati ya Zamalek dhidi ya mabingwa wa Angola Cabo Schrob. Fujo hizo zilipelekea kwa kukamatwa kwa mashabiki 33.

Tupia Comments