Michezo

Matokeo haya yameirudishia matumaini Yanga kushinda Kagame Cup 2015…

on

DSC_0067

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Gor Mahia, Yanga ilikuwa katika wakati mgumu wa kuweza kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua inayofuata… Yanga leo hii imepata ushindi wa kwanza katika mechi yake ya pili ya michuano ya Kombe la Kagame 2015 baada ya kuifunga Telecom ya Djibout.

pluijm

Yanga imepata ushindi wa goli 3-0 mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, magoli ya Yanga yalifungwa na washambuliaji waliosajiliwa msimu huu Malimi Busungu ambaye amefunga magoli mawili dakika 26, 68 huku bao la tatu likifungwa na Geofrey Mwashiuya aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo na kupachika goli la tatu dakika ya 73, mchezo uliomalizika kwa Simon Msuva na Amissi Tambwe kukosa penati.

DSC_0865

Yanga imerudisha matumaini kwa mashabiki wake ambao walikuwa na mashaka kama ingepoteza mechi ya leo kwani nafasi ingekuwa finyu kusonga mbele… Yanga sasa imebakiwa na michezo miwili kati ya KMKM ya Zanzibar July 24 2015 Uwanja wa Taifa na mchezo wa mwisho dhidi ya Khartoum ya Sudan.

Yanga-fans-to-go-to-polls

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments