Michezo

Matokeo ya mchezo wa Yanga vs Nacional Al Ahly

on

MAF3Klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans leo imefanikiwa kushinda mchezo wa kwanza wa hatua ya raundi ya pili CAF Champions League dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Nacional Al Ahly ya Egypt.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam uliotawalia kwa kiasi kikubwa na Yanga ambao walipoteza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza na mpaka timu zinaenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Yanga walionekana kutafuta bao kwa nguvu, mpaka kufikia dakika ya 50 tayari walishapata kona tisa ambazo hazikuzaa matunda. Wakati muda ukizidi kuyoyoma na mashabiki wa Yanga wakiwa wameanza kukata tamaa ya kupata ushindi dhidi ya waarab, Nadir Haroub Cannavaro aliwainua maelfu ya mashabiki wa Yanga katika dakika ya 82 baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza.

Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho ubao wa matokeo ulikuwa unasomeka 1 kwa moja na 0 kwa waarabu. Timu hizi zitarudiana jijini Cairo wiki mbili zijazo.

Tupia Comments