Michezo

Matokeo ya Al Ahly vs Yanga Misri yako hapa.

on

MBIOOOOKlabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika baada ya kufungwa katika mchezo wa raundi ya pili na mabingwa watetezi wa kombe hilo Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo uliochezwa huko Alexandria Misri ndani ya dakika 90 uliisha kwa Yanga kufungwa 1-0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1, Yanga walishinda 1-0 Dar wiki moja iliyopita.

Baada ya dakika 90 kumalizika na zile tano za nyongeza, refa aliamuru ipigwe mikwaju ya penati ambapo Al Ahly wakapata 4 na Yanga wakafanikiwa penati 3.

Waliopata Yanga Didier, Canavaro, Okwi huku waliokosa ni Oscar, Bahanuzi na Twite ambapo kwa haya matokeo sasa hivi Al ahly wanafuzu kuelekea hatua ya 16 bora.

Tupia Comments