Michezo

VPL: Unamjua Coutinho wa Yanga – hiki ndicho alichowafanya Prisons leo taifa

on

 Mshambuliaji wa Yanga, Jenilson Santos ‘Jaja’ akijikunja kupiga shuti mbele ya beki wa Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Beki wa Tanzania Prisons, akiokota mpira wavuni hili lilikuwa ni bao la kwanza.
Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Andrey Coutinho katika dakika ya 38, bao la pili lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 69, huku bao la Prisons likifungwa na Ibrahim Kahaka, katika dakika ya 67.
 Simon Msuva (kulia) akijaribu kutoka beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona, wakati wa mchezo huo.
 Simon Msuva (kushoto) akikimbia kushangilia bao lake alilofunga katika dakika ya 69.
 Sehemu ya mashabiki wa Tanzania Prisons….
Jenilson Santos ‘Jaja’ (kulia) akijaribu kupiga shuti mbele ya mabeki wa Prisons. Lugano Mwangama na Nurdin Chono. 
Picha zote kwa hisani ya sufianmafoto.com

Tupia Comments