Michezo

Ripoti na matokeo ya mechi ya Yanga vs Azam hii hapa

on

_MG_4020Vilabu vya Yanga na Azam vimetoka sare ya 1-1 katika mchezo uliomalizika hivi punde katika dimba la uwanja wa taifa.

Yanga ndio walioanza kuliona lango la Azam FC baada ya Didier Kavumbagu kuifungia timu yake katika dakika ya 14. Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana zamu kwa zamu, na wakati mashabiki wa Yanga wakiwa na uhakika wa kuondoka uwanja wa taifa wakicheka, kijana mdogo wa miaka 19 Kelvin Friday alifumua shuti kali lilotinga wavuni na kuisawazishia timu yake ya Azam.

Mpaka refa anapuliza filimbi ya mwisho matokeo yalikuwa Yanga 1-1 Azam. Kwa matokeo haya Azam imeendeleza record yake ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu msimu huu.

Tupia Comments