March 12 klabu ya Dar Es Salaam Young African ya Tanzania ilishuka katika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda kucheza mchezo wake wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao timu ya jeshi APR ya Rwanda.
Yanga imeaingia kucheza raundi ya pili ya michuano hii, baada ya kuitoa klabu ya Circle de Joachim ya Mauritius. Katika mchezo wa raundi ya pili Yanga ilifanikiwa kuitambia APR ya Rwanda kwa kuifunga jumla ya goli 2-1, licha ya kuwa APR ilikuwa nyumbani na kupata sapoti kubwa ya mashabiki wanajeshi.
Magoli ya Yanga yalianza kufungwa dakika ya 21 baada ya Juma Abdul kupiga faulo na kufunga kwa kushuti kali, hiyo ilikuwa baada ya Donald Ngoma kuchezewa faulo. Thabani Kamusoko alirudi wavuni dakika ya 75, wakati jitihada za APR ziliishia kuzaa goli moja tu dakika ya 90 kupitia kwa Patrick Sibomana.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE