Baada ya klabu ya Azam FC inayoshindana kwa karibu na klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuwania nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi kutoa sare ya 1-1 dhidi ya African Sports January 16, katika mchezo uliochezwa Azam Complex Mbande Chamazi, January 17 ilikuwa zamu ya Yanga kuikabili Ndanda FC ya Mtwara uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Yanga ambao ndio wenyeji wa Ndanda FC katika dimba la Taifa, walikutana na wakati mgumu kidogo, kwani ngome ya ulinzi ya Ndanda FC haikuwa nyepesi kupenya washambuliaji wa Yanga, hadi dakika ya 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika matokeo yalikuwa 0-0.
Kipindi cha pili licha ya kutopata nafasi sana, Yanga walibadilika zaidi na kuhakikisha wanacheza katika eneo la Ndanda FC, mbinu ambazo ziliwapeleke Yanga kupata penati mbili, penati ya kwanza Yanga walipata baada ya Simon Msuva kufanyiwa faulo katika eneo la hatari, lakini Amissi Tambwe alikosa.
Hali bado iliendelea kuwa mbaya kwa Ndanda FC, kwani Yanga walikuwa tayari wana urafiki na eneo la 18 la Ndanda FC, kwani walifanikiwa kupata penati ya pili dakika ya 60 baada ya Deus Kaseke kufanyiwa faulo katika eneo la hatari, Kelvin Yondani ndio aliamua kupiga na kupachika mpira nyavuni, hadi dakika 90 zinamalizika Yanga 1-0 Ndanda FC. Kwa matokeo hayo Yanga wanakaa kileleni mwa Ligi Kuu, kwa jumla ya point 36 sawa na Azam FC lakini Yanga wamewazidi magoli Azam FC.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.