Michezo

Hapa ndipo Yanga na Haruna Niyonzima walipofikia, kuhusu zile stori za kuvunjwa mkataba …

on

Baada ya uongozi wa klabu ya Dar Es Salaam Young African kutangaza kuwa imevunja mkataba na kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima, January 17 kiungo huyo akiwa katika makao makuu ya klabu hiyo, pamoja na afisa habari wa Yanga Jerry Muro, alitangaza kuomba radhi wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga mbele ya waandishi wa habari kutokana na kosa alilolifanya.

Licha ya kuwa afisa habari wa Yanga Jerry Muro kutotangaza rasmi kuwa klabu imemsamehe, na kusema kuwa isubiriwe taarifa rasmi, dalili zinaonesha kuwa uongozi wa Yanga na Niyonzima umeyamaliza.

Yanga walitoa barua kwa umma ya kuvunja mkataba na Niyonzima December 28 2015, barua ambayo inaeleza makosa ya Niyonzima ambayo yamepelekea haya yote kutokea. Unaweza pitia barua ya Yanga iliyotolewa December 28 2015 na mkuu wa idara ya habari wa klabu hiyo.

haruna-1

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments