Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limepitia ombi la chama cha wanasoka Tanzania SPUTANZA, TFF ambayo ilipokea ombi la SPUTANZA kushughulikia madai ya muda mrefu ya wachezaji wa zamani wa Yanga, ambao waliachwa wakati wakiwa bado wanaidai klabu hiyo. December 24 mwenyekiti wa SPUTANZA Musa Kisoki alithibitisha kupatiwa ufumbuzi suala hilo.
Wachezaji wanaoidai Yanga ni Jerson Tegete, Omega Seme, Hamisi Thabeet na Said Bahanuzi, wachezaji hao wote kwa pamoja wanadai fedha zao za usajili ambazo hawakumaliziwa na klabu hiyo, baada ya kuingia mkataba wa kuitumikia hadi kuachwa kwao, kupitia kwa mwenyekiti SPUTANZA Musa Kisoki amethibisha Yanga kupewa agizo la kulipa deni hilo kutoka kwa kamati ya haki na hadhi za wachezaji.
“SPUTANZA tuliandika barua kuiomba kamati iingilie kati madai ya wachezaji walioachwa na Yanga, kamati imeamua kuwa Yanga iwalipe wachezaji, kamati imetoa maelekezo kwa TFF kuwaandikia Yanga kuwa wanapaswa wawalipe wachezaji, kwani ni pesa zao halali na kama hawatofanya hivyo watakatwa katika mapato yao ya mlangoni katika mechi zao” >>> Musa Kisoki
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.