Mara nyingi hutokea kwenye mashindano yoyote kuna mtu au watu utakua unawahofia pengine kulingana na viwango sawa vya uchezaji au wao kukuzidi maarifa kidogo,hiko ndicho kilichotokea kwa Nyota toka Manchester City mchezaji Yaya Toure ambaye ameshinda kwa mara ya tatu mfululizo tuzo ya mchezaji bora barani Afrika,ushindi ambao umekosolewa na maafisa wakuu wa soka nchini Nigeria.
Toure mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni raia wa Cote d’Ivoire alishinda pia tuzo ya Shirikisho la Soka barani Afrika – CAF, mwaka wa 2011 na 2012 huku John Obi Mikel wa Nigeria ambaye anachezea klabu ya Chelsea ya Uingereza akichukua pili na nafasi ya tatu ikishikwa na Didier Drogba kutoka huko huko Cote d’Ivoire.
Hiki ndicho alichokizungumza Toure baada ya kutangazwa mshindi ‘Kwa kweli ilikuwa vigumu sana kushinda,kwa sababu kulikuwa na wapinzani wakali mbele yangu Obi Mikel na Didier Drogba kwa hivyo nilidhani nitashindwa na sasa nimebahatika na nina furaha kwa mafanikio yangu Ninapenda kile ninachofanya’
Muda mfupi baada ya kutangazwa ushindi huo wa Toure Maafisa wakuu wa soka nchini Nigeria waliukosoa utaratibu uliotumiwa kumpata mshindi,Utaratibu uliotumika ni wa Makocha wa timu 54 za mataifa wanachama wa CAF huwapigia kura wachezaji 10 wanaoteuliwa kwa mizani ya pointi moja hadi kumi, huku atakayepata pointi nyingi ndiye anayeondoka na tuzo hiyo.
Toure alikusanya jumla ya pointi 373 na akapigiwa kura na makocha 28 na kumpa mchezaji huyo wa Manchester City ya Uingereza ushindi wa tatu mfululizo baada ya kunyakua taji hilo mwaka wa 2011 na 2013 huku Kiungo wa Chelsea Mikel, akiwa pili na jumla ya pointi 275.