Katika Maadhimisho ya Siku ya Nyerere leo October 14, 2017, ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Rais John Magufuli amezungumza mambo yafuatayo akiongoza maadhimisho hayo katika Uwanja wa Amani Zanzibar.
"Baba wa Taifa alitamka 'Madini yetu ni vema tukayaacha mpaka Watanzania watakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba'"@MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Sambamba na hayo Serikali iliweka mkazo kwenye Elimu, ilitoa elimu bure bila ubaguzi kuanzia shule za msingi hadi Chuo Kikuu." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Mwalimu Nyerere aliamini kuwa kumkomboa mtu mnyonge ni lazima uumpe elimu." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Alihimiza watu kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia kaulimbiu za Uhuru na kazi, siasa ni kilimo." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Pamoja na misingi mizuri iliyowekwa na Baba wa Taifa kupitia Azimio la Arusha, miaka michache ya kung'atuka, tulilitupa." Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Sijui ilitokea kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Mimi sijui ila ukweli ni kwamba, tumelitupa." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Baada ya kulitupa tukaanza kuuza Mashirika na Viwanda vyetu." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Kwa takwimu tulizo nazo jumla ya viwanda 197 vimekufa na kubaki magofu. Mara nyingi huwa najiuliza ni nani hasa aliyeturoga." @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Kwa nini tuliamua kuuza viwanda vyetu? Ikawaje tukaruhusu Shrika letu likabaki na Ndege moja?" – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
"Swali ninalojiuliza kila wakati, ni kwa nini tuliliacha Azimio la Arusha wakati maudhui na misingi yake haikuwa mibaya?" – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) October 14, 2017
Ulipitwa na hii? Wakili aliyejitokeza kumuunga RAIS JPM uteuzi Katibu wa Bunge