AyoTV

VIDEO: Kauli ya Rais Magufuli kwa wanaodai ndege mpya hazina speed

on

Leo September 28 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amezindua ndege mpya mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Uzinduzi wa ndege hizo za kisasa zilizotengenezwa nchini Canada, umefanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amezungumzia uwezo wa ndege hizo huku akitoa kauli kwa wanazibeza ndege hizo ……..

>>>’Ukitumia ndege ya Jet kutoka hapa mpaka Songea utatumia milioni 28.9 za kununua mafuta, ukitumia ndege hii ni milioni moja kwa hiyo kwa watu wanaofanya biashara lazima waipige vita na utofauti wa kufika ni dakika 20, dakika 20 ukichelewa wewe zinakuuma nini na ndio maana yule aliyezungumza anataka speed akapande za jeshi’

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUZITAJA HUJUMA ZILIZOKUWEPO KATIKA SHIRIKA LA ATCL? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments