Mwimbaji kutokea nchini Kenya Akothee ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Baraka’ aliyomshirikisha Linex ametangaza kuokoka amethibitisha hilo kupitia mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha Kiss FM 100 cha Kenya .
Akothee amekiri na kusema kuwa tangu atembelee eneo la Turkana mwezi uliopita na kujionea hali ya watu kukumbwa na janga la njaa pamoja na ukosefu wa maji ilimuumiza na hivyo kutoa msaada wa chakula na ndipo hapo alipoamua kuokoka lakini hilo halitamfanya kubadilisha mavazi yake.
“Kuanzia nimefika kutokea Turkana mimi ni mtu mpya sasa, watu waliniona nafanya Injili asubuhi na hawakujua huu mwaka umekuja na nini, nimeokolewa lakini sitobadili mavazi yangu, nilitoka tumboni kwa mama yangu mtupu “ >>>Akothee
VIDEO: LULU DIVA KUOLEWA/ AROBAINI YA RUGE/ ALIKIBA AMUONYESHA MTOTO WAKE