Habari za Mastaa

Kama ulidhani Chris Brown ndiye mwenye tattoo kubwa kichwani, subiri uione hii ya YG!

on

Ukiniambia nitaje wasanii watano wa Marekani wenye tattoo kupita kiasi mwilini, kwenye orodha yangu majina haya hayatokosekana; Lil Wayne, Birdman, Chris Brown, Tyga na Wiz Khalifa.

Miezi michache iliyopita nilikusogezea picha ya tattoo mpya ya Chris Brown kichwani, tattoo iliyoleta maneno mengi sana kwa mashabiki kwenye mtandao wa Instagram… sasa kama ulidhani kuwa Lil Wayne, Tyga, Chris Brown na Wiz Khalifa ndio wasanii wenye tattoo kubwa zaidi basi ningependa kuisogeza kwako hii mpya kutoka  rapper YG!

YG2

Rapper YG.

Rapper YG ameongeza tattoo mpya kichwani ya Bikira Maria na nukuu ya mstari kutoka kwenye Biblia, kitabu cha Isaya 54 : 17 uliosema; “Hakuna silaha itakayofanyika juu yangu itafanikiwa… “

YG

Tatttoo mpya ya rapper YG kichwani ya Bikira Maria!

Kwa sasa YG yupo studio anakamilisha album yake mpya iliyopewa jina Still Krazy, na ukiacha hayo rapper huyo kaanzisha lebo yake mwenyewe ya muziki alioipa jina 4HUNNID na msanii wa kwanza chini ya lebo hiyo anategemea kutambulishwa rasmi mwaka 2016 mwanzoni.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments