Michezo

DONE DEAL: Simba SC imehakikisha John Bocco haondoki

on

Club ya Simba SC imeonekana kuonesha dhamira ya kweli ya kudhibiti mastaa wake wote waliomaliza mikataba kuwa hawaondoki ndani ya club hiyo, pamoja na kudaiwa club ya Azam FC ilikuwa inamshawishi nahodha wao wa zamani John Bocco alejee kikosini kwao baada ya kuondoka miaka miwili iliyopita.

Simba SC imefanikiwa kumbakisha nahodha wake John Bocco ambaye mkataba wake ulikuwa umemalizika, Simba SC imefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili nahodha wao John Bocco aliyekuwa amemaliza mkataba na Simba SC alikuwa anawindwa na Azam FC.

John Bocco alijiunga na Simba SC kama mchezaji huru miaka miwili iliyopita akitokea Azam FC aliyokuwa kadumu nayo kwa muda mrefu na kuipandisha Ligi Kuu, hadi msimu wa 2018/2019 unamalizika John Bocco alikuwa miongoni mwa wafungaji bora wa Simba SC kwa kufunga magoli zaidi ya 14.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments