Michezo

PICHA: Chelsea yatwaa Kombe la Europa League kibabe vs Arsenal

on

Club ya Chelsea ya England licha ya kupata changamoto kwa kukosekana kwa mashabiki wake katika mchezo wa fainali ya Europa League dhidi ya Arsenal kutokana na timu hizo kutoka umbali mrefu hadi Baku, game imechezwa Azerbaijan na Chelsea kuondoka na Ubingwa wa michuano hiyo.

Chelsea imeifunga Arsenal kwa magoli 4-1, magoli ambayo yalifungwa na Oliver Giroud dakika ya 17, Pedro dakika ya 60, Eden Hazard aliyefunga mawili dakika ya 65 kwa penati na dakika ya 72 huku Arsenal wakipata la kufutia machozi kupitia kwa Iwobi.

Rekodi yake Unai Emery aliyoiweka dhidi ya Sevilla ya kutwaa mara tatu mfululizo Kombe hilo 2014, 2015 na 2016, haijaweza kumsaidia Unai Emery na hatimae anaondoka kwa kipigo kikubwa na Chelsea kudhiirisha ubabe kutokana na kutwaa Ubingwa huo kwa idadi kubwa ya magoli.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments