Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

Shabiki wa Simba aliyetembea kwa mguu kutoka Mbeya hadi DSM kuifuata TP Mazembe

on

Moja kati ya habari inayosambaa katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu ni habari ya Shabiki wa Simba SC wa jijini Mbeya Shaban Ramadhani aliyeamua kuja jijini Dar es Salaam kwa miguu, kwa ajili ya kuja kuisapoti timu yake ya Simba SC katika mchezo wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumamosi ya April 6 2019.

Shabiki huyo amekuwa gumzo mitandaoni kutokana na uamuzi wake huo wa kutembea kwa miguu karibu wiki nzima kuja Dar es Salaam kuisapoti Simba, kigezo ikiwa ni kutokana na timu hiyo kufanya vizuri sasa hivi na kumfurahisha, hivyo alivyofika maeneo ya Kibaha alichangiwa pesa na mashabiki wa Simba SC, safari hiyo aliianza March 26 2019.

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments