Michezo

Yanga SC yaanza kwa ushindi bila uwepo wa Zahera VPL

on

Ikiwa zimepita siku chache toka Yanga SC chini ya mwenyekiti wao DR Mshindo Msolla imfute kazi aliyekuwa kocha wao Mwinyi Zahera, leo Yanga SC walikuwa Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona kuikabili Ndanda FC.

Yanga wamefanikiwa kuondoka na point tatu muhimu kutoka Mtwara baada ya kupata ushindi wa 1-0, kwa goli lililofungwa na Patrick Sibomana dakika ya 75 ya mchezo na kuwafanya Yanga wafikishe point 10.

Baada ya mchezo huo Yanga SC watarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko mafupi ya Ligi kupisha mechi za kimataifa, kabla ya Ligi Kuu Tanzania bara kuendelea tena November 25 2019.

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

Soma na hizi

Tupia Comments