Top Stories

Tamthiliya ya Game of Thrones yavunja rekodi ndani ya msimu wake wa 8

on

Inaripotiwa kuwa tamthiliya ya Game of Thrones (GOT)  imeweka rekodi kubwa ya watazamaji katika episode yake ya kwanza kwenye msimu wa 8 kwa usiku mmoja na kufikisha kiwango cha watazamaji jumla ya milioni 17.

Inaelezwa kuwa Game of Thrones imevunja rekodi yake ya awali ikiwa Episode 1 ya msimu wa 7 ilifikisha kiwango cha watazamaji milioni 16.5 mwaka 2017 na hivyo kuweka rekodi mpya mwaka huu 2019  na kuwa episode ya kwanza iliyotazamwa zaidi kwa muda wote kupitia kituo cha televisheni cha HBO.

Tamthiliya ya Game of Thrones inatajwa kuachiwa rasmi mwaka 2011 kupitia televisheni ya HBO na kuelezwa kuwa mapokezi ya tamthiliya hiyo yalifikia asilimia 95 ya kipindi hicho kupendwa na watu wengi na kufuatilia tamthiliya hiyo.

VIDEO: ULIPITWA NA MARAFIKI WALIVYOCHOKA KUOMBWA LIFT NA MWENZAO, WAMNUNULIA GARI LAKE? BONYEZA PLAY KUTAZAMA HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments