Habari za Mastaa

Mwigizaji mkongwe Mama Abdul afariki dunia leo

on

Mwigizaji maarufu nchini Salome Nonge ‘Mama Abdul’  inaripotiwa kuwa amefariki dunia leo January 25,2019 baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa ini.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mchekeshaji  Joti ametoa taarifa za kifo cha Mwigizaji huyo mkongwe kwenye tasnia ya Bongo movie nchini baada ya ku-post picha na kuambatanisha na ujumbe >>>R.I.P Mama Abdull Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama..🙏🙏”

Salome Nonge maarufu kama Mama Abdul alijiunga na kundi la Kaole Sanaa Group miaka kadhaa nyuma na alijizolea umaarufu mkubwa kupitia tamthilia mbalimbali ikiwemo  Kanitangaze, Mambo hayo na ameonekana kwenye kipindi cha vichekesho cha Mwantumu akiwa na Joti.

MAHABA YA BARNABA NA MAMA MTOTO WAKE YAMEANZA KURUDI UPYA..?

Soma na hizi

Tupia Comments