Tasnia ya filamu Tanzania ambayo wengi tumeizoea kwa jina la Bongo Movie inazidi kupiga hatua kila siku kutokana na waandaaji kuzidi kufuata mifano ya nchi zilizoendelea katika upande wa Film Indrustry, Muigizaji Simon Mwapagata ambaye wengi tuna mfahamu kwa jina la Rado ameeleza kuhusia na project yake.
Rado amethibitisha kuwa filamu yake ya Bei Kali ataizindua October 4 2017 katika ukumbi wa Mlimani City Cinema ambapo ndani yake kuna wasanii kama Duma, Irene Uwoya na Hemed PHD, kingine cha tofauti ni kuwa movie hii mpya production imefanywa na Kwetu Studio.
“Kikubwa nimefanya production ya tofauti na tuliyozoea kutumia, kwa sasa wamefanya Kwetu Studio pia format tuliyoshoot ya safari hii ni tofauti na tuliyozoea kwa sasa tumeshoot 4K hivyo nikaona kuna sababu ya kuipeleka Movie kwenye Big Screen hususani pale Mlimani City”>>>Rado
VIDEO: Petman baada ya picha yake na Hamisa Mobetto kusambaa mitandaoni