Michezo

PICHA: James Msuva kafanyiwa vipimo nchini Morocco

on

Baada ya kaka mtu Simon Msuva kumuombea ruhusu mdogo wake katika club ya KMC na kwenda nae nchini Morocco kwa ajili ya kumpatia matibabu zaidi.

Leo James Msuva amefanyiwa kipimo kikubwa na kuchunguzwa zaidi kuhusiana na tatizo lake la nyama za paja, ambalo limekuwa likimuweka nje mara kwa mara, majibu ya vipimo yatatoka kesho.

Simon Msuva ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco, baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Burundi aliamua kuondoka na mdogo wake na kwenda kumtibia nchini Morocco kwa gharama zake.

Soma na hizi

Tupia Comments