Habari za Mastaa

Khloe Kardashian akanusha taarifa za kumnyakua Tristan kwa Jordan Craig

on

Mwanadada Khloe Kardashian ameweka wazi kuhusu mahusiano yake yaliyopita na mchezaji wa kikapu wa NBA Tristan Thompson na kusema kuwa sababu kubwa iliyomfanya kuingia kwenye mahusiano hayo ni baada ya kuambiwa kuwa Tristan aliachana rasmi na aliyekuwa mpenzi wake.

Khloe Kardashian aliandika ujumbe huo kupitia kwenye insta story baada ya kuwepo na tuhuma kuwa mpenzi wa zamani wa Tristan ambaye ni Jordan Craig kudai kuwa mpenzi wake alianzisha mahusiano mengine na Khloe kipindi akiwa mjamzito na kudai kuwa alimuuliza Tristan kuhusu tetesi hizo lakini alikana.

“Ukweli ni kwamba Nilikutana na Tristan na aliniambia kuwa ameachana na mpenzi wake na alinionyesha mpaka uthibitisho hata mama yake mzazi alinithibitishia hilo niliamini hicho, naomba sana msamaha kama Tristan na watu wake walidanganya kuhusu hilo, Mungu anajua naomba na kutoka moyoni naomba msamaha kwa maumivu ambayo yamejitokeza hakuna mwanamke ambaye anastahili kupitia wakati mgumu, huu ndio ukweli wangu” aliandika Khloe

Jordan Craig alibahatika kupata mtoto wa kiume pamoja na Tristan Thompson mwaka 2016 na  April 12,2018 Khloe Kardashian na Tristan walipata mtoto wa kike ambaye anafahamika kwa jina la True Thompson hata hivyo Khloe Kardashian na Tristan waliachana rasmi mwezi February mwaka huu.

VIDEO: UMEPITWA NA HAYA MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUMUHUSU IDI AMIN UTABAKI MDOMO WAZI! BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments