Habari za Mastaa

Vifahamu Vigezo anavyoangalia Young Killer kwenye Collabo zake.

on

IMG-20140107-WA0004Unaweza kuwa na ndoto za kutamani kumshirikisha Serengeti Fiesta Super Nyota 2012/13 Young Killer kwenye wimbo wako ambao unadhani anaweza kufit vizuri,millardayo.com imeongea na Young Killer  kuhusu muziki wake kwa ujumla ikiwa ni pamoja gharama anazotoza kwenye kushirikishwa.

IMG-20140107-WA0001Young Killer amesema mpaka sasa ameshaitwa kwenye Collabo nyingi sana lakini anashindwa kufanya kutokana na ubovu wa Beat wa sehemu anazoitwa kashaitwa mara kadhaa lakini mwisho wa siku anashindwa kufanya kitu kwa sababu ya beat kuhusu pesa amesema hatozi gharama kubwa ila anachoangalia zaidi ni beat.

Collabo ambazo kafanya mpaka sasa anasema hazizidi 5,collabo zake haangalii mwenzake kaimba nini ila anachokiangalia ni beat na kama ikiwa poa basi mwisho wa siku point zile 3 zote zinaenda kwake,kuhusu video ya Mrs.Superstar amesema wanategemea kuiachia kuanzia wiki ijayo.

Tupia Comments