Michezo

Wewe ni wa Yanga? Full Time ya Yanga vs Mgambo JKT ninayo hapa kama ulimis

on

Screen Shot 2014-11-08 at 11.06.49 PMBaada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba, November 8 2014 Yanga imejitupa uwanjani vs Mgambo JKT kwenye uwanja wa taifa Dar ea Salaam.

Mpaka Full Time Yanga ikachukua ushindi wa goli 2-0 japo game ilikua ngumu kwa timu zote na mpaka kufikia dakika 25 za mwisho hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzie lakini muda mfupi baadae Simon Msuva akaifungia Yanga goli la kwanza.
IMG_8674.JPG

Kwenye dakika za majeruhi kabisa akaongeza goli la pili ambalo lilihitimisha ushindi wa Yanga dhidi ya Mgambo ambao waliifunga Yanga lakini msimu uliopita.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments