Habari za Mastaa

Adele amtolea nje Beyonce kwenye collabo?! sababu? Beyonce amelipokeaje hili!

on

Msanii yoyote akifatwa sasa hivi na kuambiwa “Beyonce anataka kufanya collabo na wewe..” kwa asilimia mia jibu litakuwa ndio tena kwa herufi kubwa NDIO!! Lakini hii sio ndoto kubwa kwa msanii wa muziki wa Pop kutoka Uingereza, Adele.

Kwa mujibu wa baadhi ya mitandao ikiwemo mtandao wa Yahoo Celebrity News, umeripoti kuwa Beyonce amekuwa akiomba kufanya kazi na staa huyo wa Uingereza kwa takribani mwaka mzima lakini juhudi zake hazijawahi kuzaa matunda, inaripotiwa pia kuwa, Beyonce alishaingia studio na Adele na kujaribu kumshawishi staa huyo kurekodi nae wimbo mwaka jana lakini bado Adele akamtolea nje.

BEYADELE2

Adele & Beyonce Knowles.

Licha ya hayo, tunaambiwa toka kipindi hicho Beyonce amekuwa akijaribu mara kwa mara kubadilisha mawazo ya Adele ili kuingia naye studio, lakini kila mara anapojaribu Adele anakataa, kitendo kilichompelekea Beyonce na yeye kufanya maamuzi ya kuirekodi single hiyo mwenyewe na kuiweka kwenye Album yake mpya inayotegemea kuwa mtaani mwishoni wa mwaka 2015.

>>> “ Bey amekuwa akimuomba Adele kwa kipindi kirefu kuingia naye studio na pamoja kuweka historia nyingine kwenye muziki, akafanikiwa kumleta studio lakini alipojaribu kumshawishi kuhusu kurekodi naye wimbo Adele alikataa kabisa, kwahiyo Beyonce naye ameamua kuuweka wimbo huo kwenye Album yake mpya, na inawezekana Album hiyo ikatoka mwisho wa mwaka huu…” <<< source karibu na Beyonce aliuambia mtandao wa Heat Magazine.

BEYADELE3

Adele.

Na kwa mujibu wa mtandao wa International Business Times, Adele ametoa sababu za yeye kukataa kufanya kazi na Beyonce Knowles

>>> “ Nadhani kazi zake na historia yake kama msanii na muimbaji inaogopesha na kutoa changamoto kubwa… lakini watu wengi wanaonivutia mimi na ambao ningependa kufanya nao kazi ni watu wa old school music na kwa bahati mbaya wote wametangulia mbele za haki, isitoshe sivutiwi na umaarufu kwa sababu naogopa umaarufu unaweza kunipoteza kimuziki na vilevile naogopa kuiumiza familia pamoja na watu wangu wa karibu, mpaka hapa nilipofika bado napata shida kuzoea…” <<< Adele.

BEYADELE4

Adele na Beyonce ni wasanii wawili ambao ushawishi wao duniani ni mkubwa sana na licha ya wao kufanya aina mbili tofauti za muziki, mastaa hawa wameweza kupata umaarufu mkubwa kwa kusimama peke yao kimuziki na licha ya mashabiki wao kuonekana kuvutiwa na wazo la wawili hao kufanya collabo, tunaambiwa Beyonce hana kinyongo na msanii huyo.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments