Habari za Mastaa

Baada ya taarifa ya kumteka Msichana,Hiki ndicho alichokisema Ney wa Mitego.

on

neyApril 14 zilizotoka taarifa juu ya kutekwa kwa msichana mmoja aitwae Neema ambaye ni miongoni mwa watu wanaosemekana walimtukana Ney na Mpenzi wake kupitia akaunti zao za Instagram,Neema alipatikana na kuzungumzia hii bahati mbaya Ney hakuwa nchini aliporudi Soud Brown kaongea nae na hiki ndicho alichokisema.

Ney ameanza kwa kusema>>’Mimi sijawahi kuteka mtu,zamani labda muda mrefu wakati wa maisha ya kimtaa zile vurugu za kimanzese manzese lakini kwa sasa mimi siwezi kuthubutu kumteka mtu kanifanya nini,maisha ya kizamani hivyo vitu vilikuwa vinatokea lakini kwa sasa siwezi kusema nimemteka fulani’

‘Mimi ni Star naanzaje kufanya hivyo huyo Bonge wanamsingizia tu hawezi sidhani kama aliwahi kufanya kama alifanya hivyo sijui kilimnufaisha nini na sidhani kama alifanya hivyo,Tar 14 nilikuwa Mozambique na nina uhakika’

‘Matusi yanakera kwenye Instagram lakini najua mimi ni Star angekua Juma Msagasumu wala wasinge comment hivyo vitu au wasingetukana siku hizi mitandao haina nidhamu tunaona watu wanatukanwa kama Rais na Mawaziri’

‘Huyo mtu simjui ndiyo maana nasema mkampime akili mimi sielewi kinachoendelea,mimi nipo kwa ajili ya kufanya muziki sio kwa ajili ya kushindana na watu,mimi nawapenda sana wanawake naamini wanawake wote wanajua’

‘Mimi nishawaimbiia wanawake mi napenda Wanawake wakifanya maendeleo wanawake wote mimi ndiyo mashabiki zangu kwanini leo nianze kufanya hivyo lakini napenda kumrekebisha Mwanamke akikosea,huyo Gresi mimi simjui’.

96.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tanga.

Bonyeza play kusikiliza.

Tupia Comments