Habari za Mastaa

Sababu inayosemekana ya Babu Tale kumsimamia Shilole kikazi kwa sasa ni hii.

on

shilole1Manager wa Tip Top Connection na Diamond Platnumz Babu Tale inasemekana anamsimamia kwa sasa Shilole kama msanii wake kwa kile ambacho kimeelezwa na Soudy Brown kuwa deni alilokua anadaiwa Shilole.

Deni ambalo linasemwa kuwa Babu Tale alilipa ni la gari ambalo alikua akidaiwa Shilole hivyo wakakubaliana kuwa watakua wakikatana kwenye show tofauti mpaka deni hilo litakapoisha.

Soudy Brown kaongea na Shilole ambaye kasema ‘Mbona mimi sijui hayo mambo,sio kweli huo uwongo watu waongo sio kweli,gari ni langu na nina kila kitu changu watu wana donge kuona mimi Shilole naendesha Toyota Harrier Lexus nilinunua Milion 24’

‘Babu Tale ni mtu anayenisaidia kwenye kazi zangu na namheshimu kama kaka yangu nimeanza nae kazi mwaka huu na sina mkataba nae’.

Tupia Comments