Habari za Mastaa

Maneno ya Stamina baada ya kushindwa kutokea kwenye show ya Mabeste.

on

staaWiki chache zilizopita kulikua na show iliyoandaliwa na Mabeste ambayo aliifanya Club Bilicanas miongoni mwa wasanii waliotajwa kuwepo kwenye show hiyo ni pamoja na Stamina lakini kutokana na sababu ambazo zilikua nje ya uwezo wake hakuhudhuria,Mabeste alisikika akilaumu hali hii,kwa hapa leo msikilize Stamina.

Hapa anaongea Stamina na Soudy brown>>’Hayo mambo yote yanakuja kutokana na mimi kutohudhuria kwenye show yake au vipi yaani maana yake maana hizo lawama zote mi zisielewi,kuhusu yeye kuja kwenye show yangu Morogoro kufanya free ndiyo makubaliano yetu yalivyokuwa kama ambavyo mimi ilitakiwa nije kwa show yake ilikua kishkaji’

‘Mimi sikumwambia nipo Masaki nilimwambia nipo Mbezi lakini hakunipigia na kutaka kujua tatizo gani tena mimi lilinitokea,kuna tatizo lilinitokea la kifamilia zaidi hakunipigia kujua mimi kitu gani kilinipata yeye alikua anaangalia mimi kuja kwenye show yake’

Soudy Brown:Ulipata tatizo gani hilo?

‘Mambo mengine ya kifamilia zaidi siwezi kuyasema hivi yeye kama alitaka kujua ukweli angenipigia simu kujua tena hakuna kitu ambacho kimenishangaza kwa yeye kuja kwenye radio na kusikia sijui kaongea nini na kumuonyesha mimi nina busara sana sikumpigia hata simu kwa kumuuliza umeongea nini radioni’

‘Kuna vitu vingi sana tunaongeaga chini ya carpet angeniambia tu alitakiwa anipigie simu mimi mwenyewe tunakua tunatafuta nini majina redioni au nini?

Soudy Brown:Hamna yeye ilimuuma zaidi baada ya kukatwa asilimia 75 na Bilicanas halafu ukizingatia wewe mshkaji wake wa karibu amekutengenezea beat’

Stamina:Beat ya Lango la jiji ni yeye Mabeste na Kev walikua studio pamoja kwani nilienda kufanyia chumbani kwake,si alienda kufanyia studio kwa Kev tulienda kwa Kev,siku tumeenda kufanya kazi na Mabeste Kev alikua ameshaanza kutengeneza Beat Mabeste nae anapiga Beat wakaongezea ujuzi wote kwenye hiyo beat kuna shukrani hajapewa kwenye hiyo nyimbo ‘

‘Hiyo nyimbo inatoka wiki ijayo tumefanya mimi(Stamina),Stereo pamoja na Jux tumeandika kabisa imetengezwa na Kev pamoja na Mabeste sasa tatizo nini hapo’

Soud Brown:Lakini Stamina hukumpa taarifa yoyote hata meseji kumpa taarifa kuwa hautofika.

Sikia nikwambie,sitaki kuzungumza mimi kitu kilichonitokea ni kikubwa sana siwezi kukizungumza hivi,huo muda tu wa kushika simu wenyewe nilikua sina tatizo watu wanajali sana kufanyiwa kazi zao bila kujali hizi kazi zipo tu,show zipo tu,hela zipo tu,kuna vitu vinaitwa afya’

‘Sasa afya yangu mimi unaweza ukainunua,kilitokea kitu mimi mtu mmoja katika familia yangu alipata tatizo nikawa mmojawapo wa watu wanaotakiwa kupatia ufumbuzi tatizo,nilitakiwa kuchagua vitu viwili kati ya mshkaji au ndugu wa damu’

104.1 Clouds Fm inasikika ukiwa Bukoba.

Bonyeza play kusikiliza.

Tupia Comments