Duniani

Rubani mdogo wa kike na rekodi zake alivyorusha ndege Marekani akiwa na miaka 15.. (+Video)

on

Kuna wakati unaweza usione kipaji au uwezo wa mtoto wako, lakini kuna umuhimu mkubwa kuwa karibu na mtoto kwa sababu anaweza kuwa na kipaji na uwezo mkubwa kuliko vile ambavyo unafikiria..

Nakumbuka mtoto wa Marekani aliyebuni saa, akaenda nayo shule wakahisi bomu… akaitiwa Polisi, baadae kesi yake ikaisha na hakuwa na hatia, lakini kila mtu alimpongeza na kuusifu ubunifu wake !! Hakufundishwa kutengeneza saa, aliibuni mwenyewe.

Nakupa na hii kutoka Marekani, inamhusu msichana Kimberly Anyadike ambaye wazazi wake mmoja ana asili ya Marekani, mwingine ni Mnigeria.

Kimberly

Ndoto yake ilikuwa afanikiwe kurusha Ndege akiwa anaiendesha yeye mwenyewe, ndoto yake ilitimia July 2015 ambapo alitoka na Ndege Compton, akazunguka California, mpaka Newport News, Jimbo la Virginia kwa siku 13 akiwa na ndege ndogo.

kim-anyadike

Msichana huyo alijifunza kurusha ndege kuanzia akiwa na miaka 12 nyumbani kwao Compton… Wakati wa safari yake kuivunja rekodi hiyo, pembeni yake alikuwepo pia Rubani mwenye uzoefu mkubwa, Levi Thornhill ambaye alimsimamia kwenye safari yote.

Kujiamini ni kila kitu mtu wangu, video ya story yake hii hapa mtu wangu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments