Habari za Mastaa

Young Thug anasemaje kuhusu kupenda kuvaa nguo za kike? Mapenzi ya jinsia moja je!?

on

Msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani, Young Thug anajulikana kwa kazi zake nyingi za muziki lakini pia anajulikana zaidi kwa tabia yake ya kupenda kuvaa nguo za kike, kitu ambacho kimeleta maneno mengi sana juu ya rapper huyo huku wengi wakidai pengine labda rapper huyo anachochea mahusiano ya jinsia moja!

THUG2

Rapper Young Thug.

Kwa muda mrefu sana Young Thug amekuwa akisita kufanya interviews na Radios pamoja na majarida mbalimbali kuhusu vitu hivi, lakini hivi karibuni rapper huyo alikubali kufanyiwa interview na jarida la The Guardian, na miongoni ya maswali alioulizwa ni kwa nini anapenda sana kuvaa nguo za kike na je anavutiwa na wanawake ama wanaume zaidi! Rapper huyo alikuwa na haya ya kusema…

>>> ” Kwanza napenda kuvaa nguo za kike kwa sababu zinanikaa freshy sana, nguo za kike zinakuja kwenye size ileile nayoitaka mimi haswa jeans, jeans zangu zote ni za kike hata hii nilioivaa na kama kuna kitu chochote cha kiume kwenye kabati langu la nguo basi itakuwa ni T-shirt zangu na raba tu lakini asilimia 99 ya nguo kabatini mwangu ni  nguo za kike… “<<< Young Thug.

THUG3

Young Thug akiwa amevaa skin jeans na top, vyote vya kike!

Alipoulizwa anavutiwa na jinsia gani zaidi kimapenzi, rapper huyo alikuwa na haya ya kusema…

>>> “navutiwa kusikiliza kila kitu ambacho watu wanasema na kukiongelea juu yangu, haijalishi wanasema nini. Niwe napenda watu wa jinsia moja, niwe kichaa, niwe na demu mkali, niwe mbaya, labda waseme sijui kurap… vyote mimi naenjoy kuvisikiliza tu, nawaacha waongee.” <<< Young Thug.

THUG1

Design kama Young Thug alikwepa kujibu swali hilo kwa kudai kuwa yeye anasikiliza tu maneno yote yanayozungumzwa na watu juu yake, lakini kitu ambacho amekiweka wazi bila kuficha ni kwamba, yes anapenda kuvaa sana nguo za kike kwa sababu zinamkaa vizuri mwilini!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.

 

Soma na hizi

Tupia Comments