Top Stories

Bilionea mwenye miaka 59 aoa binti wa miaka 19

on

Mwigizaji maarufu kutokea NollyWood Regina Daniel mwenye umri wa miaka 19 amechukua headlines nchini Nigeria baada ya kuolewa na Bilionea maarufu nchini humo Ned Nwoko mwenye umri wa miaka 59 miezi kadhaa iliyopita.

Waigizaji mbalimbali wamejitokeza kumtetea Regina kuhusu umri uliopo kati ya mwigizaji huyo na Ned Nwoko ambapo baadhi ya watu wamedai kuwa Regina anamtumia Bilionea huyo kama chombo cha kukuza uchumi ndani ya familia yake pamoja na yeye binafsi kutumia nafasi hiyo kuchuma mali. 

Mwigizaji Helen Paul akiwa miongoni mwa Waigizaji waliomtetea Regina Daniel kupitia mtandao wa Instagram ambapo kwa upande wake alihoji maswali mengi na kusema kuwa nchi ya Nigeria ina vitu vingi vya kuzingatia kuliko kelele zinazoendelea kwenye mitandao kuhusu ndoa hiyo.

“Unafki kuhusu umri mkubwa, wasichana wamezoea kuuana wenyewe. Mnajua alichopitia? unajua ni nini kimemsukuma yeye pamoja na familia yake mpaka kujiingiza kwenye masuala ya ndoa? Kuna watu wanaolewa wakiwa na umri mkubwa na waume zao wanawatumia kama mifuko ya kupigwa”

“Mbona ni wepesi kuhukumu wanawake? mwanamke alifanya hivi, alifanya vile vipi kuhusu wanaume? Tafadhali tuache mambo ambayo yanarekebishwa na tuzingatie yale yanayohitaji hasa unakini zaidi. Nigeria ni kubwa mno na ina vitu vingi vya kutatua, kila mtu ni mdhambi?” >>> Helen Paul

VIDEO: BALAA LA MWIMBAJI NANDY WAKATI AKIIMBA WIMBO WA NINOGESHE NAIROBI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO 

Soma na hizi

Tupia Comments