Michezo

Matokeo ya Yanga vs Kagera Sugar haya hapa pamoja kilichotokea kwenye mechi ya Azam vs Ruvu

on

DSC_6109Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga ya Dar es salaam leo imepata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar, Yanga waliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli kupitia Hamis Kiiza katika dakika ya 3 tu mchezo.

Didier Kavumbagu aliiongezea Yanga goli la pili kwenye mchezo  huo katika dakika ya 34 na mpaka mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 64, Kagera wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Daudi Jumanne.

Katika hatua nyingine mchezo wa Azam FC dhidi ya Ruvu uliokuwa ukifanyika huko Mlandizi ulihairishwa kutokana na mvua kubwa iliyoonyesha na kuharibu uwanja – mchezo huo sasa utapigwa kesho.

Tupia Comments