Michezo

DoneDEAL: Coutinho kaondoka FC Barcelona

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania leo imetangaza rasmi kumuachia staa wake wa kimataifa wa Brazil Philippe Coutinho kwenda kujiunga na club ya FC Bayern ya Ujerumani kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kununuliwa jumla mwisho wa msimu wa 2019/20.

Coutinho amejiunga kwa mkopo na FC Bayern watatakiwa kuilipa FC Barcelona euro milioni 8.5 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 21 na endapo watamtaka jumla mwakani basi watalazimika kulipa kiasi cha euro milioni 120 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 306.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Philippe Coutinho alijiunga na FC Barcelona 2018 akitokea Liverpool ya England aliyokuwa amedumu nayo kwa miaka mitano (2013-2018), Coutinho mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa hana nafasi kubwa ya kucheza katika club ya FC Barcelona.

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments