Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Kuna story Yaya Toure hana uhusiano mzuri na Uongozi wa Man City? Ni kweli ana mpango wa kuhama ?

on

Yaya Boy

Msimu wa ligi si wa mafanikio kwa Manchester City baada ya klabu hiyo kushindwa kutetea taji lao la ligi kuu ya England ambalo walitwaa msimu uliopita na pia wameshindwa kwenda mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora.

Kingine ambacho huenda sio taarifa nzuri kwa Klabu ya Manchester City ni taarifa za kuondoka kwa kiungo wao kutegemewa, Yaya Toure.

Dimitri Seluk ambae ni wakala wa kiungo huyo raia wa Ivory Coast, Yaya Toure amevithibitishia vyanzo mbalimbali vya habari hii kuwa mteja wake ana uhakika wa 90% kuihama klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Wakala huyo amefichua kuwa uhusiano wa Yaya na Manchester City umekuwa mbovu na imefikia hatua mbaya kiasi cha mchezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoka na kufikia uamuzi ambao hawezi kuubadilisha.

Itakumbukwa kuwa kiungo huyo aliingia kwenye ugomvi ambao uliripotiwa sana kwenye vyombo vya habari mwaka jana wakati klabu yake iliposhindwa kumfanyia hafla ya siku yake ya kuzaliwa wakati City ilipokuwa kwenye ziara ya huko Falme Za Kiarabu ripoti ambazo baadae zilikanushwa.

Yaya Toure amehusishwa na kuungana na kocha wake wa zamani Roberto Mancini anayefundisha klabu ya Inter Milan .

Yaya Toure  na kocha wake wa zamani Roberto Mancini anayefundisha klabu ya Inter Milan.

Wakati hayo yakiendelea Yaya Toure kwa nyakati kadhaa amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na kocha wake wa zamani Roberto Mancini ambaye kwa sasa anaifundisha Inter Milan.

Kwa upande wa uongozi wa Man City inasemekana kuwa klabu hiyo inajiandaa kusikiliza ofa zitakazokuja kwa ajili ya mchezaji huyo kutokana na umri wake kusogea huku uongozi ukiwa na mpango wa muda mrefu wa kujenga kikosi cha City kwa kuwategemea zaidi wachezaji wenye umri mdogo.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments