Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil aliyejiunga na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kwa rekodi ya uhamisho wa dunia akitokea FC Barcelona Neymar, ameamua kumuomba radhi mchezaji mwenzake Edinson Cavani kwa kilichotokea wakati wa game dhidi ya Lyon.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Neymar na Cavani walionekana kama kutokuwa katika maelewano wakati wa mchezo huo, baada ya kuonekana mwanzoni Neymar kutaka kupiga penati aliyopiga Cavani na baadae Danny Alves kuonekana akimnyima Cavani mpira wa faulo na kumpa Neymar.
Hata hivyo kocha wa Paris Saint Germain Emery akiongea na waandishi wa habari alipoulizwa kuwa ni nani anatakiwa kupiga penati na faulo, alijibu kuwa wote wanastahili kupiga penati na kukataa kutaja nani ni chaguo la kwanza ila habari zilizoripotiwa na gazeti la L’EQUIPE kuwa Neymar alimuomba radhi Cavani.
KAMA HUKUONA TUKIO LA NEYMAR NA CAVANI TAZAMA HAPA
https://youtu.be/1OFG7-hVeHk
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC leo Sept. 21 Mwanza (2-2)