Bara la Afrika linafahamika duniani kwa shughuli za kilimo kama msingi wake mkubwa wa maendeleo yake ya uchumi na inatabiriwa kuwa kufikia mwaka 2050 Afrika itaweza kulisha dunia nzima.
Hii inatokana na ongezeko la watu linalotarajiwa kuongezeka kufikia bilioni 9.1 ambapo uhitaji wa chakula pia utaongezeka sana na Afrika kutokana na kilimo chake inauwezo wa kufanikisha hilo. Hata hivyo imeelezwa kuwa hili litafanikiwa kama mambo matatu yafuatayo yatafanyika
1.Kuwekeza kifedha katika sekta hiyo
Serikali za nchi za Afrika ni lazima zitenge bajeti kubwa kwa ajili ya sekta ya kilimo ambazo zitasaidia kutoa mikopo kwa wakulima kwa ajili ya uzalishaji ili mavuno yenye ubora yaongezeke.
Inaelezwa kuwa uwekezaji mkubwa katika kukiboresha kilimo kutoka ngazi ya chini kutaongeza matokeo makubwa sana ya sekta hiyo na kunufaisha watu wake.
2. Kuwekeza zaidi katika vijana
Wataalamu wa uchumi wanaeleza kuwa kama nchi za Afrika zitawekeza nguvu nyingi katika vijana ili wajihusishe katika kilimo na kukifanya kiwe chanzo kikubwa cha mapato yao, sekta hii italeta mapinduzi makubwa.
3. Teknolojia
Pia mapinduzi ya uchumi kupitia kilimo yataratibiwa kwa haraka sana na matumizi ya teknolojia katika sekta hiyo. Teknolojia mpya zitasaidia kuongeza ufanisi na ubora wa shughuli zote za kilimo suala litakalo endeleza sana kilimo.
Ulipitwa na hii? Kama una mpango wa kulima mbogamboga, kuna hii ya kufahamu