Habari za Mastaa

(PICHA) Taraji P. Henson atunukiwa nyota yake Hollywood Walk of Fame

on

Mwigizaji  Taraji P Henson hatimaye amekabidhiwa nyota yake siku ya January 28,2019 kwenye Hollywood Walk of Fame akiwa miongoni mwa waigizaji waliotoa mchango mkubwa katika jamii kwenye upande wa filamu.

Inaelezwa kuwa nyota hiyo ni ya 2597 kutolewa kwenye eneo hilo kwa watu maarufu na wenye mchango tofauti katika jamii. Mwigizaji huyo hakuweza kujizuia na kuangusha chozi alipokua akitoa shukrani zake kwa mashabiki waliosababisha yeye kutunukiwa nyota hiyo.

 

Taraji P Henson >>> “Napenda kuwashukuru mashabiki zangu, nisingekuwa hapa kama sio nyie nazidi kuangalia hii nyota siamini kama ni kweli, kila kitu nachofanya ni kwaajili ya watoto, nina mtoto wa kiume na sikutaka kukata tamaa kwa sababu ningekuwa namfundisha nini mwanangu……”

 

 

Imekuwa ni desturi kwa mastaa mbalimbali nchini Marekani kutunukiwa nyota hizo kutokana na mchango mkubwa waliotoa kwenye jamii na pengine kutokana na kuwepo kwenye game ya filamu au muziki kwa muda mrefu na kufanya vizuri.

 

ULIPITWA NA MASTAA WALIOFIKA MSIBANI NYUMBANI KWA MAMA ABDUL?

Soma na hizi

Tupia Comments