Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Rapper Fabolous aumbuka, message zake zaanikwa

on

Rapper maarufu kutokea Marekani Fabolous aumbuliwa na message alizomtumia mrembo matata kupitia insta direct baada ya kumuuliza sehemu anapoishi na mwanadada huyo kusema kuwa hapendi watu waongo na kwa sasa ni mchumba wa mtu.

Mrembo huyo anayejulikana kwa jina la Fiorella Zelaya ameweka wazi mazungumzo aliyotumiwa na rapper huyo kupitia mtandao wa instagram ikiwa jumbe hizo ni direct message na ukitupilia mbali kuumbuka kwa rapper Fabolous mrembo huyo amefunguka na kusema kuwa ana viwango vya juu na sio video vixen wa kuchukuliwa kawaida.

Fabulous na mzazi mwenzake Emily B

Inadaiwa kuwa tukio la rapper Fabolous  kuachana na mzazi mwenzake Emily B kwa kumpiga na baadae kurudiana linaonekana bado kumuumiza hadi kufikia hatua ya kufanya kitu kama hicho kupitia mtandao wake wa instagram.

Picha za mrembo Fiorella Zelaya aliyemuumbua Rappa Fabolous kwenye ukurasa wa instagram.

HISTORIA: HIVI UCHUNGAJI WA PASTOR MYAMBA UMETOKEA WAPI?

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments