Habari za Mastaa

Kingine alichoandika Vanessa juu ya tour INLOVE & MONEY Mwanza

on

Wakali kutokea kwenye Bongo Fleva Vanessa Mdee pamoja na Juma Jux ambao pia ni wapenzi wanakuja na tour yao ya Inlove & Money ikiwa inahusisha album ya Juma Jux inayoitwa Inlove na album ya Vanessa Mdee ambayo ndio Money Mondays (Inlove &Money).

Tour hii itahusisha mikoa mbalimbali na pia wasanii ambao wapo chini ya record label ya Mdee Music watapewa nafasi ya kuperform katika mikoa hiyo, mkoa wa kwanza kuhusishwa ni Rock City Mwanza ambapo Vanessa Mdee pamoja Juma Jux watawasili na kutoa burudani June 30,2018.

“Kwanza Kabisa Thanks To The Lord najiona kabisa nikitua #Mwanza#Fimbo ake mtu #ILAM #MapenziNaPesaThe Vanessa Mdee and Jux Tour. Leo tutaanza kutambulisha wasanii watakao ungana nasi Mwanza. Wewe unataka kumuona nani pale kati? #InLoveAndMoneyTour

Mkoa wa Mwanza ndio utafungua tour hiyo ya Inlove & Money ikiwa ndio itakua mara ya pili kwa Vanessa Mdee pamoja Juma Jux kufanya performance katika mkoa huo ambapo mara ya kwanza ilikuwa kwenye Fiesta 2017.

“Gigy Money is not my Type, siwezi kuwa na tatizo na mtu ambaye yupo chini yangu”

Soma na hizi

Tupia Comments