Top Stories

Jamaa anaeongoza duniani kuwa na tattoo nyingi (+video)

on

Leo January 12, 2020 Kuna hii ya kuifahamu ni kumhusu Lucky Diamond Rich mwenye miaka 49, ndiye mtu mwenye tattoo nyingi mwilini mwake kwa rekodi ya mwaka 2019.

Mbali na michoro aliyonayo, pia ametoboa masikio na kuyavuta (kama Wamasai), na meno yake ameweka madini ya fedha (Silver), pia amejitoboa sehemu kadhaa za mwili wake.

Alianza kujiweka michoro mwilini mwake akiwa na umri wa miaka 16, kwa kuwa kazi yake ni maonyesho aliendelea kujichora hadi akawa mtu anayeshikilia rekodi ya kuwa na michoro mingi.

Alimaliza kujichora mwili wake akiwa na umri wa miaka 28 na akaanza kuboresha michoro aliyo nayo.

Lucky hajajiweka michoro mipya kwa takriban miaka 6 na bado hakuna aliyekuja kuvunja rekodi yake.

MAGUFULI ASHTUKIZA HOSPITAL ZANZIBAR AKUTA WATOTO WAKIWA HOI “MBONA HAWAHUDUMIWI”

Soma na hizi

Tupia Comments